Chuo cha Ustawi wa Jamii

WAFANYAKAZI BORA WATUNUKIWA VYETI

Wafanyakazi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii wa muda mrefu, kutoka idara mbalimbali na wabunifu watunukiwa Vyeti. Hafla ya kuukaribisha Mwaka mpya na kufanya tathimini ya Mwaka 2023 ulimpa fursa Mkuu wa Taasisi kutunuku Vyeti kwa watumishi waliofanya kazi kwa muda mrefu, wabunifu pamoja na waliofanya vizuri katika idara na vitengo mbalimbali. Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii Dr. Joyce Nyoni kabla ya ugawaji wa vyeti hivyo alimesema “Kila Mtu anamchango mkubwa katika ukuwaji na mafanikio ya Taasisi, hivyo tungetamani kila Mtu aweze kupata zawadi lakini tutawapatia wachache walionekana kufanya zaidi’’.

Wanawake Watumishi ISW Waigusa Jamii

Katika Matukio mawili tofauti Wanawake Watumishi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii wametoa Zawadi na Elimu katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani. Wanawake Watumishi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii Kampasi ya Kisangara, Mwanga Kilimanjaro wametembelea Shule ya Sekondari Nyerere na kutoa Elimu kwa Wanafunzi pamoja na zawadi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Taulo za kike. Kwa Upande wa Kampasi ya Kijitonyama, Dar es Salaam Watumishi Wanawake wametembelea Shule ya Watoto wenye mahitaji Maalum ya "Sinza Maalumu" iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam na kutoa zawadi na bidhaa mbalimbali za mahitaji muhimu. Matukio haya yamefanyika tarehe 05 na 06 Machi 2024.

ISW YAENDESHA MAFUNZO YA PROGRAMU WEZESHI KWA WANAFUNZI WENYE UONI HAFIFU

Chuo cha Ustawi wa Jamii kupitia ofisi ya mshauri wa wanafunzi kimefanikiwa kuandaa na kuendesha Mafunzo ya Programu wezeshi kwa wanafunzi wenye Changamoto ya uoni (wasioona). Program hii imefanyika mwishon mwa Mwezi Februari mwaka 2024 na imejumuisha jumla ya Wanafunzi nane wanaosoma katika Chuo cha Ustawi wa Jamii pamoja na wasaidizi wanne kwa ajili ya kuwaongoza Wanafunzi wenzao wasioona katika maeneo mbalimbali na kufanya programu hii kujumuisha Jumla ya washiriki kumi na mbili. Mafunzo haya ya Programu wenzeshi wameendeshwa chini ya Mkufunzi Honolath Ngowi kutoka katika Chuo Huria (Open University). Dhima kuu ya Mafunzo haya ni kuwawezasha Wanafunzi wasioona kuweza kuendana na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia yanayokuwa kwa kasi kila iitwapo leo. Katika mafunzo haya wanafunzi wamejifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ustadi katika matumizi sahihi ya kibodi wakati wa matumizi ya kompyuta.

Maendeleo ya Kasi Kampasi ya Kisangara

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Wakili Amon Mpanju amekipongeza Chuo cha Ustawi wa Jamii kwa Maendeleo ya kasi yanayoendelea katika Kampasi ya Kisangara. Wakili Amon Mpanju ametoa pongezi hizo wakati wa Mahafali ya 6 ya Chuo cha Ustawi wa Jamii Kampasi ya Kisangara, Mwanga Kilimanjaro Januari 26, 2024. ambapo jumla ya wahitimu 237 wametunukiwa tuzo mbalimbali. "Naipongeza pia Menejimenti ya Chuo kwa kusimamia vizuri ujenzi wa Hostel mbili zenye ukubwa wa kubeba wanafunzi 208, ujenzi wa mgahawa kwa matumizi ya wanafunzi na jamii nzima inayozunguka chuo. Nawapongeza pia kwa juhudi ambazo mmezichukua za kuhakikisha maji yanapatikana katika eneo letu la Chuo. Hakika hii itaifanya Kisangara iendelee kuwa ya kijani zaidi." Amesema Mpanju. Mpanju pia amefurahishwa na kuanzishwa kwa kozi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto kwa ngazi ya cheti na diploma ambayo inatambuliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET), kuanzishwa kwa programu ya Shahada ya Ustawi wa jamii (Bachelor Degree in Social Work) inayotambuliwa na Tume ya Vyuo vikuu Tanzania (TCU) katika mwaka wa masomo 2023/2024 Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Mhe. Abdalah Mwaipaya akizungumza katika mahafali hayo amesema uwepo wa chuo cha Ustawi wa Jamii Kisangara ni muhimu kwa wilaya ya mwanga kwa kuvutia zaidi uwekezaji. Amewaasa wanafunzi kurudi Mwanga Kuendelei kusoma Chuo cha Ustawi wa Jamii Kampasi ya Kisangara. Naye Naibu Kamisha wa Ustawi wa Jamii Tullo Masanja amewakumbusha wahitimu kuwa ndiyo madaktari wa jamii kutokana na ongezeko la tatizo la afya ya akili, hivyo wanatakiwa kutumia utaalamu waliopata kuhakikisha wanalinda na kuokoa jamii, hasa mmomonyoko wa maadili. Dkt. Lulu Mahai (Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Magavana ya Chuo) Ameeleza Jinsi ambavyo kampasi inakabiliwa na changamoto ya jengo la utawala na ufinyu wa jengo la maktaba ukizingatia ongezeko la wanafunzi baada ya kuongeza Programu mbili za Kitaaluma katika kampasi hiyo.

KONGAMANO LA 10 LA KITAALUMA LAJADILI ujenzi wa ujuzi na ushirikishwaji wa watu wenye wenye mahitaji maalum katika shughuli za maendeleo

Wadau, wanataaluma na wanafunzi wameshiriki katika kongamano la 10 la kitaaluma (Convocation) juu ya ujenzi wa ujuzi na ushirikishwaji wa watu wenye wenye mahitaji maalum katika shughuli za maendeleo. Akizungumza leo Desemba 7, 2023 jijini Dar es Salaam wakati akifungua kongamano hilo , Naibu Mkuu wa Chuo Prof.Sotco Komba Taaluma amesema chuo kimejikita zaidi katika maboresho ya watu wenye ulemavu ili kukuza ujuzi katika nyanja ya maendeleo ya kiuchumi ili waweze kushirikia michakato mbalimbali ya maendeleo katika taifa letu. Dkt. Nassib Mwaifunga, mtaalam wa masuala ya Uchumi na Fedha na Sheria kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu amewataka vijana kuchangamkia fursa mbalimbali kutoka ofisi ya Waziri Mkuu hasa walemavu ili waweze kujikomboa kiuchumi na kukuza maeneleo katika maisha yao ya kila siku. Aidha aliwataka vijana ambao ni wanafunzi kwenda na wakati katika mafunzo na masomo wanayochukua ili waweze kwenda na kasi ya soko la ajira duniani. Amebainisha fursa kubwa hasa ajira ambazo zinapewa kipaumbele kwa kuzingatia ujuzi iko katika kiwango kikubwa katika kozi za mafuta na gesi, usafirishaji, afya na vifaa tiba na madini. Mbali na hilo amewataka waajiri nchini kuachana na dhana ya kudharau watu wenye mahitaji maalum hasa katika kuwapa ajira kwani watu hao wana uwezo mkubwa wanapopewa nafasi. #chuochaustawiwajamii kimepongezwa kwa kuanzisha kitengo maalum utoaji wa huduma kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum na ni mfano wa kuigwa na vyuo vingine nchini Umekuwa ni utamaduni wa Chuo cha Ustawi wa Jamii kufanya kongamano hili la kitaaluma kila mwaka kabla ya mahafali yake, ambapo kwa mwaka 2023 mahafali hayo yatafanyika tarehe 08/12/2023 katika ukumbi wa JKT mwenge.

ISW Yashinda Tuzo Uandaaji Taarifa za Hesabu za mwaka 2022

Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii Dkt. Joyce nyoni akiwa pamoja na baadhi ya wahasibu wa #ISW akipokea tuzo ya mshindi wa tatu ya uandaaji wa taarifa za hesabu chini ya viwango vya IPSASs 2022, katika kundi la vyuo vya elimu ya juu nchini kwa mara nyingine. Tuzo hiyo imetolewa jioni ya tarehe 1, Disemba 2023 na NBAA katika hafla maalum ya kutoa tuzo hizo.

BONANZA LA MICHEZO KUELEKEA KILELE CHA MIAKA 50 LAZINDULIWA

Dkt. Happy Mwakajila kwa Niaba ya Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii Dkt. Joyce Nyoni amefungua Bonanza la Michezo ikiwa ni sehemu ya shughuli mbali mbali kuelekea Kilele cha Miaka 50 ya Chuo ambapo timu ya Mpira wa Miguu ya Wanaume #ISW imepimana nguvu na timu ya watumishi wa Hospitali ya Ocean Road Dar es Salaam ambapo timu zote mbili zimetoka sare ya bila kufungana katika mechi hiyo. Michezo hiyo itakutanisha Taasisi na vyuo mbali mbali ikihusisha wanafunzi na watumishi katika michezo mbali mbali.

NAIBU KATIBU MKUU WAKILI AMON MPANJU AFANYA KIKAO KIFUPI ISW

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Wakili Amon Mpanju amefika katika Chuo cha Ustawi wa Jamii leo tarehe 10/11/2023 na kukutana na baadhi ya Wajumbe wa Menejimenti ya chuo ili kupata taarifa ya hali ya utoaji huduma, maendeleo ya miradi ya chuo na vile vile kutoa maelekezo na ushauri katika kuboresha utoaji huduma na utekelezaji wa miradi ya chuo.

CHUO CHA USTAWI WA JAMII CHAFANYA MAWASILISHO YA TAFITI ZA KITAALUMA.

Chuo cha Ustawi wa Jamii leo tarehe 10/11/2023 kimefanya mawasilisho ya tafiti mbili za kitaaluma ambazo imezifanya katika mada mbili tofauti ikilenga kutafuta kina cha suluhu ya matatizo ya hali mbali mbali yanayotokea katika jamii ya kitanzania. Akiwasilisha taarifa za tafiti hizo mmoja wa mtafiti kiongozi wa tafiti hizo Mhadhiri Mwandamizi Dkt. Zena Mabeyo amesema wamefanya tafiti mbili ambazo ni: - ‘’kuchunguza kanuni, maadili na mbinu zinazowalinda wanawake dhidi ya unyanyasaji Tanzania: uchunguzi kesi ya mikoa ya Mbeya, Mara na Tanga’’ na kuathirika kwa wafanyakazi wasio rasmi katika muktadha wa Uviko 19: kesi ya sekta ya utalii mkoani Kilimanjaro na Arusha. Kwa taarifa Zaidi tembelea ; https://www.isw.ac.tz/assets/doc/Dissemination_brief_PROWOMEN.pdf, https://www.isw.ac.tz/assets/doc/REPOA_FINAL_EDITED_POLICY_BRIEF_07_11_2023_(1).pdf

KARIBUNI - ISW

Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii Dkt. Joyce Nyoni amefungua Mafunzo ya awali kwa watumishi wapya ISW. Akiongea katika ufunguzi wa mafunzo hayo katika kampasi ya Dar es Salaam, Dkt. Joyce amewapongeza watumishi hao wapya na kuwaasa kuwa waadilifu, wachapakazi, kufanya kazi kwa weledi, na kutoa huduma bora kwa wateja wa Chuo cha Ustawi wa Jamii.

Announcements
Fill in NHIF required information 2024-01-23 12:27:20
Test Timetable. ISW-Kisangara Campus. 2024-04-29 09:29:11
Semester 2 TestTimeTable2023-2024 2024-04-25 12:57:09
Class sessions Timetable. ISW - Kisangara Campus 2024-04-16 12:46:28
First Semester Supplementary Examinations for Students Who Got Below 2.0 GPA for NTA Level 4-9 Academic Year 20232024 2024-04-12 04:47:29
TimeTable Semester II Main Campus Fourth Draft 2024-04-09 05:49:14
ALMANAC 2024 - 2025-MARCH INTAKE- KISANGARA CAMPUS 2024-04-05 12:50:30
Class Sessions Timetable ISW - Kisangara Campus 2024-03-17 07:01:12
...BTCSW - JOINING INSTRUCTION MARCH INTAKE KISANGARA CAMPUS 2024-2025 2024-03-15 12:10:46
ODSW JOINING INSTRUCTION MARCH INTAKE KISANGARA CAMPUS 2024-2025 2024-03-15 12:10:19
SELECTED CANDIDATES TO JOIN CERTIFICATE AND DIPLOMA PROGRAMMES AT ISW (MARCH INTAKE) -KISANGARA CAMPUS 2024-03-15 12:09:18
Call for Proposals 2024-02-19 09:59:49
CALL FOR JOURNAL ARTICLES 2024-02-19 09:58:44
Examination Regulations 2023-2024 Edition 2024-02-16 06:03:35
Examination Time Table Updated 09.02.2024 2024-02-09 07:47:54
Open for March Intake Applications - Kisangara Campus 2024-02-07 13:27:59
SEMESTER ONE EXAMINATIONS TIMETABLE FOR SEPTEMBER INTAKE 2023.2024. KISANGARA CAMPUS 2024-01-31 06:44:19
First Semester Examination TimeTable 2024-01-10 07:17:04
Third draft Time table -Institute of social work Kisangara Campus 2024-01-02 19:20:06
TEST EXAMINATION TIME TABLE ACADEMIC YEAR 2022/2023 - DECEMBER 2023-12-12 12:15:56
Second Semester Examination Time Table Match Intake 2023-11-17 14:28:54
Wasilisho la Utafiti wa Kitaaluma - Exploring Norms, Values and Approaches that Protect Women Against Abuse in Tanzania: Case Study of Mbeya, Mara and Tanga Regions. 2023-11-10 13:35:13
Wasilisho la Utafiti wa Kitaaluma - Buffering Deprivation and Vulnerability among Informal Workers in the Covid-19 Context: The Case of the Tourism Sector in Kilimanjaro and Arusha 2023-11-10 11:38:08
April - June 2023 Newsletter 2023-10-12 06:03:37
2022/23 - 2023/24 Academic Almanac (All Programs) 2023-09-26 06:57:04
Fee Structure 2023-09-21 00:00:00
Site Visitors
Today
500
Yesterday
599
This Week
6,024
This Month
33,175
All days
248,623
Online
2
Video